STREETLIB KENYA

StreetLib Kenya is a publishing portal for authors and publishers in Kenya to digitally distribute their books around the world, with no up-front fees.

Books can be published in English and most other languages, and will be distributed to ebook retailers and digital libraries worldwide, including to the world’s biggest ebook retailers like Amazon, Google Play, Kobo and Apple.  

StreetLib Kenya ni kampuni ya uchapishaji iliyo kwenye mtandao ya kuwasaidia waandishi na wachapishaji kusambaza vitabu vyao ulimwenguni kote bila ada yoyote.

Vitabu vinaweza kuchapishwa kwa lugha ya Kiingereza na kwa lugha zingine nyingi. Vitabu hivi vitasambazwa kwenye maduka yanayouza vitabu pepe (e-books) na maktaba za kidijitali duniani kote. Hii ni pamoja na maduka makubwa zaidi duniani kama Amazon, Google Play, Kobo na Apple.  

WHAT IS STREETLIB?

StreetLib is a global gateway distributor of digital books, based in Italy, and serving authors and publishers worldwide. 

Established in 2006, StreetLib has the widest international reach of any digital distributor. Authors and publishers can make their books digitally available to readers in almost every country in the world, and get paid for every sale. There are no upfront fees - StreetLib simply deducts a 10% commission from net and pays you the rest.

JE, STREETLIB NI NINI?

StreetLib ni kampuni ya wasambazaji wa kimataifa wa vitabu vya kijiditali walio nchini Italia. Huwa wanahudumia waandishi na wachapishaji duniani kote.

Ingawa kampuni hii ilianzishwa mwaka wa 2006, sasa imeenea kimataifa zaidi ya kampuni nyingine yoyote ya wasambazaji wa kidijitali. Waandishi na wachapishaji wanaweza kufanya vitabu vyao viwafikie wasomaji kwa njia ya kidigitali katika karibu kila nchi duniani na watalipwa kila mara kitabu chao kinaponunuliwa. Hutatozwa ada yoyote ila StreetLib hukata kodi ya asilimia kumi ya bei jumla ya kitabu chako, kisha wanakulipa fedha zinazobaki 

WHAT IS A DIGITAL BOOK?

At its simplest, a digital book, or ebook, is a digital file of a book or manuscript that can be bought, downloaded and read on a smartphone, an e-reader or a laptop or desktop computer by anyone anywhere in the world with an internet connection. No printing costs, no storage costs, no shipping costs.

JE, KITABU CHA KIDIJITALI NI NINI?

Kwa kifupi, kitabu cha kidijitali, ama kitabu pepe, ni faili ya kidijitali ya kitabu ama muswada ambayo inaweza kununuliwa, kupakuliwa, na kusomwa kwenye simu za kisasa, kompyuta mpakato (laptops), ama kompyuta za kawaida na mtu yeyoye duniani bora awe na utandawazi. Hakuna gharama za uchapishaji, ama gharama za uhifadhi, wala gharama za usafirishaji.

Are there enough people around the world connected to the internet to make this worthwhile?

In Kenya alone there are over 43 million people online. That’s more than Spain. That’s 10 million more than Canada. That’s twice as many as Australia and for times as many as Belgium or Sweden. At 85%, Kenya has the highest internet penetration of any country in Africa.

Your books uploaded to the StreetLib Kenya portal will be available to buy as ebooks in Kenya and across Africa via the StreetLib international store, as well as globally. There are already over 450 million Africans online.

In fact Africa has more internet users than Latin America, more internet users than the European Union, and almost 150 million more than the USA. Yet Africa as a continent is only at 35% internet penetration. So much room to grow!  

 

Je, kuna watu wa kutosha waliounganishwa kwenye mtandao ili kufanya jambo hili liwe lenye faida?

Katika nchi ya Kenya tu kuna zaidi ya milioni arobaini na nne ya watumizi wa mtandao. Nambari hii imeshinda watumizi walio katika nchi ya Uhispania. Pia, nambari hii ni milioni kumi zaidi ya watumizi wa mtandao nchini Kanada. Isitoshe, nambari hii ni mara mbili ya watumizi wa mtandao nchini Australia na mara nne ya wale walio nchini Ubelgiji au Uswidi. Nchi ya Kenya inaongoza katika upenyaji wa mtandao Afrika kote na asilimia 85. 

Vitabu vyako vikipakiwa kwenye tovuti ya StreetLib Kenya vitaweza kupatikana kama vitabu pepe (e-books) vinavyoweza kununuliwa nchini Kenya na kote Afrika, kupitia kwenye hifadhi ya kimataifa ya StreetLib. Pia, vitabu hivi vitapatikana kimataifa. Tayari kuna zaidi ya Waafrika milioni 450 kwenye mtandao.  

Kwa kweli, Afrika ina watumizi wa mtandao wengi kushinda Amerika ya Kilatini, Umoja wa Ulaya, na karibu watumizi milioni 150 zaidi ya wale wa Marekani. Na bado kuna nafasi kubwa sana ya kukua kwani kwa jumla upenyaji wa mtandao katika bara la Afrika ni asilimia 35 tu. 

Globally there are over 4 billion people online, and the global book market is valued at over $143 billion (KES 14.4 trillion).

StreetLib Kenya offers free formatting tools, if needed, to turn your book or manuscript into a digital file. Authors and publishers can upload a single book at a time, or use our batch upload option for large quantities of titles. The StreetLib Kenya upload portal dashboard is in English, Italian, Spanish, Hindi, Telegu and Tamil. But the books themselves can be uploaded in any language, including indigenous Kenyan languages like Swahili, Kikuyu, Kamba, etc, and sold through the StreetLib International store, as well as being distributed to any retailers that supports that language. StreetLib currently hosts over a quarter million ebooks. Add yours for free. Earn money from every sale.  


Kuna zaidi ya watumizi wa mtandao bilioni nne duniani kote. Nalo soko la vitabu duniani linakadiriwa kuwa na thamani ya zaidi ya dola bilioni 143 (yaani shilingi trilioni 14.4 za Kenya).  

Kampuni ya StreetLib Kenya inakupa vifaa hitajika vya kubadilisha muundo wa kitabu au muswada wako kuwa katika faili ya kidijitali bila malipo yoyote. Waandishi na wachapishaji wanaweza aidha kupakia kitabu kimoja kimoja au wapakie vitabu vingi kwa pamoja kama wana kiasi kikubwa cha vitabu.

Tovuti ya kupakia ya StreetLib Kenya inapatikana kwa lugha ya Kiingereza, Kiitaliano, Kihindi,Telegu na Tamil. Lakini vitabu vyenyewe vinaweza kupakiwa kwa lugha yoyote hata lugha za kiasilia za Kenya kwa mfano Kiswahili, Kikuyu, Kikamba na kadhalika. Hivi pia vinaweza kuuzwa kupitia maktaba ya kimataifa ya StreetLib na kusambazwa kwa maduka mengine yoyote yanayokubali lugha hiyo Kwa sasa StreetLib ina zaidi ya vitabu pepe milioni 250. Ongeza chako bila malipo ujipatie hela kwa kila mauzo. 

StreetLib. Your global gateway distributor for the 2020s.

GO TO STREETLIB

StreetLib. Lango lako la usambazaji wa kimataifa la 2020s.